Aina gani ya Injili Paulo alihubiri? Alihubiri Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Matendo 19:1-2 inasema “Ikiwa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu akafika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha huko akawauliza, Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Hata hivyo watu hawa walikuwa wamekwisha mwamini Yesu huku wakiwa wameweka kando maana ya ubatizo wa Yesu. Hawakujua juu ya Injili njema ambayo hupelekea kumpokea Roho Mtakatifu ndani. Na hii kupelekea Paulo kuuliza “Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” lilikuwa swali geni kwa baadhi ya wafuasi. Watu wengine wangeliweza kuuliza “Je, una mwamini Yesu?” Lakini Paulo aliuliza swali katika njia isiyokuwa ya kawaida ili kwamba waweze kumpokea Roho Mtakatifu, ndani yao kwa kufanya upya imani zao katika Injili njema. Huduma ya Paulo ilikuwa ni kuhubiri Injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji.
https://www.bjnewlife.org/
https://youtube.com/@TheNewLifeMission
https://www.facebook.com/shin.john.35
Katika Mwanzo 1:2 imeandikwa, “Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu na giza lilikuwa juu ya uso wa maji”. Tunaweza kuona toka katika kifungu hiki...
Mtume Paulo aliandika juu ya Roho Mtakatifu katika Waraka kwa Wagalatia. Katika Wagalatia 5:13-14 alisema “Maana ninyi, ndugu mliitwa mpate uhuru lakini uhuru wenu...
Katika kifungu kilichopita hapo juu tumeona wanawali watano wenye busara na wapumbavu, wanawali wapumbavu waliwaomba wale wenyebusara kuwagawia kiasi cha mafuta ya taa lakini...